TAARIFA YA KAMATI YA KWANZA YA UCHUNGUZI WA MADINI

Kamati moja kati ya mbili zilizoteuliwa  na Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli leo imekuja na taarifa rasmi baada ya uchunguzi uliofanyika juu ya makontena 277 ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini. Kamati hiyo ilikuwa na jukumu la kuchunguza kiasi, aina, viwango vya madini yaliyo kwenye mchanga.

Licha ya taarifa hiyo kamati pia imetoa mapendekezo baada ya taarifa hiyo.

Msoma taarifa ambaye ni mwenyekiti wa kamati Prof. Mruma alisema yafuatayo;

"Kamati ya kwanza ilihusisha wataalam wa jiolojia,kemia,uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini. Uchunguzi huo ulifanyika katika maabara za Serikali ikiwemo maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kamati imegundua kuwa mchanga uliofanyiwa uchunguzi una viwango vingi vya madini. Jumla ya makontena 277 yalifanyiwa uchunguzi, kamati iligundua kuwa kuna madini ya kimkakati ambayo ni muhimu na ya gharama lakini yalikuwa hayahesabiwi. Nyaraka za usafirishaji zinaonesha tani 4 za Shaba kwa kila kontena lakini Kamati imegundua tani 5.2 - 6.75 kwa kontena. Kiwango cha Silva kilikuwa 6kg-7kg kwa kontena moja hivyo kufanya jumla ya 1939kg kwa makontena 277 yaliyozuiwa bandarini. Kamati ilibaini thamani ya makontena 277 yaliyofanyiwa uchunguzi kuwa ni kati ya wastani wa bil.829.4- tril.1.439."

Baada ya taarifa hiyo kamati imependekeza watendaji wote wa wizara na TMAA waliohusika na mchakato huo wachukuliwe hatua.

Toa maoni yako juu ya taarifa hii.

Comments

Popular posts from this blog

SIKU YA AFRIKA