Kamati moja kati ya mbili zilizoteuliwa na Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli leo imekuja na taarifa rasmi baada ya uchunguzi uliofanyika juu ya makontena 277 ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini. Kamati hiyo ilikuwa na jukumu la kuchunguza kiasi, aina, viwango vya madini yaliyo kwenye mchanga. Licha ya taarifa hiyo kamati pia imetoa mapendekezo baada ya taarifa hiyo. Msoma taarifa ambaye ni mwenyekiti wa kamati Prof. Mruma alisema yafuatayo; "Kamati ya kwanza ilihusisha wataalam wa jiolojia,kemia,uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini. Uchunguzi huo ulifanyika katika maabara za Serikali ikiwemo maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kamati imegundua kuwa mchanga uliofanyiwa uchunguzi una viwango vingi vya madini. Jumla ya makontena 277 yalifanyiwa uchunguzi, kamati iligundua kuwa kuna madini ya kimkakati ambayo ni muhimu na ya gharama lakini yalikuwa hayahesabiwi. Nyaraka za usafirishaji ...