SIKU YA AFRIKA


Waafrika washerehekea siku ya Afrika

Siku ya Afrika ambayo mwanzo ilikuwa ikiitwa Siku ya Uhuru ya Muafrika ni sherehe za kila mwaka tangu baada ya uundwaji wa Jumuia ya nchi za Afrika (AU) zamani ukijulikana kama OAU mnamo 25 Mei 1963. Husherehekewa na nchi zote barani Afrika na Waafrika wote walio nchi mbali mbali duniani. 




Lengo la kuanzishwa kwa umoja huu ilikuwa ni kutatua matatizo ya nchi za Afrika wnyewe kwa wenyewe kiuchumi, kisiasa ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili. Wawakilishi thelathini wa nchi za Afrika walikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye mkutano ulioendeshwa na Mtawala Haile Salassie. Kwa wakati huo nchi zaidi ya theluthi mbili zilishafanikiwa kupata uhuru kutoka kwa nchi za Ulaya. Kwenye mkutano huu ndipo Umoja wa Afrika ulipoanzashwa. Lengo la kwanza la mkutano huu ilikuwa ni kuzipigania baadhi ya nchi ambazo hazijapata uhuru bado kupata. Nchi walizoanza nazo ni Angola, Msumbiji, Afrika ya Kusini na Southern Rhodesia.


Comments